Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond kawafungukia wanaobeza muziki wa Amapiano

551b9805392436492ef79df783e6e00c.jpeg Diamond Platnumz

Sun, 28 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema, wanaowabeza wasanii wanaoimba amapiano kuwa wameishiwa mawazo ni watu wasiojiamini.

Akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) juzi, msanii huyo alisema anachoamini muziki ni biashara hivyo ni muhimu kwao kuleta vionjo tofauti kuendana na soko. Alisema kwa mtizamo wake haamini kama muziki wa amapiano unaweza kuua soko la bongo fleva kwasababu wanaingia kwingine kisha wanarudi nyumbani.

“Tuache hizi mambo kuzungumza sijui amapiano na kuipoteza bongo fleva, tunaangalia soko liko wapi na kuna wakati unaweza kuingia huko kisha baadaye ukarudi kwenye bongo fleva,”alisema. Mbali na hilo, alizungumzia umuhimu wa kufanya uwekezaji wa biashara mbalimbali ili zimsaidie maisha yake ya baadaye baada ya muziki.

Diamond alisema “Lazima tuwekeze kwenye shughuli mbalimbali ili keshokutwa tuweze kutengeneza riziki,”. “Nimekuwa katika mazingira ambayo naiogopa kesho, nimejifunza kwa vijana wengi lazima tuwekeze. Kesho na keshokutwa hata usipofanya shoo tuweze kufanya kitu kuendelea na maisha,”alisema.

Kuelekea kipindi hiki cha sikukuu za Krismas na Mwaka mpya alitoa mwito kwa wasanii wenzake kuandaa nyimbo nzuri zinazoendana na majira zitakazovutia mashabiki wao sokoni akisema anaamini kila mtu ana mipango yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live