Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond kainua mashavu yangu juu - H Baba

Diamond Na H Baba Diamond kainua mashavu yangu juu-H Baba

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaweza ukacheka na kudhani ni utani lakini ndio ukweli wenyewe kutoka kwenye kinywa cha msanii Hamisi Ramadhan Baba ‘H Baba’ ambaye ametamka kuwa, bosi wa Wasafi Classic Baby, Naibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ndiye aliyemfanya mashavu yake yakue.

H Baba amefunguka hayo juzikati alipokuwa akifanya mahojiao na Wasafi FM ambapo alisema, kuna wakati baadhi ya watu walimkondesha na walitamani kumfanya awe chini lakini anamshukuru Mungu Diamond alirudisha mashavu yake.

“Yani nilipomuomba tu msamaha Diamond hapo hapo mashavu yangu yakaanza kurudi. Kuna watu walinikondesha sana na walitamani niwe vilevile,” anasema H Baba.

Licha ya kutowataja majina au jina lakini inafahamika H Baba alikuwa karibu na staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ ambaye baadaye walitofautiana na kila mtu kushika hamsini zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live