Kaka wa supastaa wa Bongo Fleva na CEO wa Konde Gang, Diamond Platnumz aitwaye Ricardo Momo amefunguka na kusema msanii ndugu yake huyo hawezi kukaa na rafiki asiekuwa na faida kwake.
Ricardo amesema kuwa, hata kwa ndugu yake na Diamond asipokuwa na faida huwezi kukaa nae wala kuonekana naye waki-hang pamoja.
"Diamond hakai na mtu karibu kwa urafiki tu kipumbavu pumbavu, hakai na mtu asiye na faida. Ukikaa naye lazima uwe na faida, hana urafiki wa kijingajinga.
"Ukiona Diamond anazunguka na mtu basi ujue ana faida kwa upande wake na huyo mtu ananufaika kupitia Diamond, hata kwa ndugu.
"Yeye hakai na mtu pasipokuwa na faida, yani faida ya pande zote mbili, mfanyie kitu yeye anufaike na wewe unufaike, hatoi sadaka tu kwa yeyote, eti ndugu njoo tuzunguke baadae uchukue uondoke, hapana," amesema Ricardo.