Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond awaburuza Davido, Wizkid

Diamond Awaburuza Davido, Wizkid Diamond awaburuza Davido, Wizkid

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa muziki wa Bongo Fleva @diamondplatnumz amekuwa msanii wa kwanza Afrika mwenye ngozi nyeusi kufikisha wafuasi milioni 8.66 kapitia mtandao wa YouTube.

Mafanikio hayo yanapelekea #Diamond kuwaburuza wasanii mbalimbali wenye ngozi nyeusi wa Afrika akiwemo Burna Boy, Davido na Wizkid.

Msanii anayefuata baada ya Diamond kuwa na wafuasi wengi ni Burna Boy akiwa na 4.65 milioni, akifuatia #Davido 3.88 milioni, #Wizkid 2.99 milioni na #Asake akiwa na wafuasi 1.09 milioni.

Aidha katika orodha iliyotolewa na tovuti ya ‘Pan African’ imeonesha kuwa mwanamuziki Diamond ni msanii wa tano kuwa na wafuasi wengi kwa Afrika nzima. Huku namba moja ikishikwa na Muigizaji na mwanamuziki wa Misri Mohamed Ramadan mwenye asili ya Kiarabu ambaye anaupiga mwingi kwenye nyimbo za Kiarabu akiwa na wafuasi 15.4 milioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live