Iringa. Mwanamuziki Diamond Platnumz amekuwa kivutio katika maonyesho ya kutangaza utalii kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutokana na shughuli kusimama kwa takribani dakika 20 wakati akitembelea banda moja hadi jingine.
Wananchi na baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo waliacha shughuli zao na kuanza kumfuatilia mwanamuziki huyo.
Hali ya utulivu katika viwanja vya Kihesakilolo yanakofanyika maonyesho hayo ilianza kutulia baada ya Diamond kuondoka eneo hilo kuelekea uwanja wa Samora linapofanyika onyesho la Wasafi Festival leo jioni Jumamosi Septemba 21, 2019.
Baada ya kuwasili uwanjani hapo alitembelea baadhi ya mabanda ya wawekezaji na alipofika katika banda lenye simba, waliokuwa karibu yake walianza kuimba, “simba, simba, simba.”
Mwanamuziki huyo pia hujiita Simba, huenda watu hao walimshangilia wakimfananisha na mnyamapori huyo.
Wapo waliomfuata nyuma wakitaka kupiga naye picha na baadhi kumtaka apande jukwaani kutumbuiza.
Pia Soma
- Alikiba arudi Shule ya Msingi Upanga
- MPYA: Mjane wa bilionea aliyeuawa Kenya anyimwa urithi
- Mke wa bilionea aliyeuawa Kenya aomba aruhusiwe kumzika mumewe