Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond avaa tshirt yenye picha ya Zuchu

Mondiii Zuu Diamond avaa tshirt yenye picha ya Zuchu

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi za msanii Diamond Platnumz kutoka kimapenzi na msanii aliye chini ya lebo yake ya Wasafi Classic Baby (WCB), Zuchu zinazidi kukolea munyu huku vielelezo na dalili zote zikiashiria hilo.

Hii ni baada ya Diamond kuonekana amevalia tisheti yenye picha ya Zuchu kwa mbele huku akiwa amejiweka vizuri kwa ajili ya kupigwa picha hiyo.

Katika picha hiyo ambayo ilivujishwa na watu mbalimbali mitandaoni, Diamond anaonekana kwenye tisheti hiyo yenye picha ya Zuchu akiwa amevalia kikofia.

Picha hiyo ilizua maoni kinzani miongoni mwa mashabiki wa wasanii hao huku wengine wakidai kwamba hakuna kubwa hapo kwani ni kawaida kuvalia nguo yenye picha ya mtu ambaye ameshakuwa staa mkubwa na si jambo geni kutokea kutoka kwenye fani ya michezo hadi sanaa.

“Kawaida tu mbona hata sisi mtaani tunavaa nguo zenye picha zake na za watu wengine kama Alikiba, Samatta, Messi, Ronaldo na wengine wengi? Hakuna ubaya eti,” mmoja kwa jina Martina Ngoni aliandika.

Wengine wanasema ndiyo mwanzo kabisa msanii huyo anapagawa kwenye penzi la Zuchu na ndiyo atazidi kuonesha viashiria vyote hadi mahasidi wakome.

“Mimi huwa nashangaa Zuchu amekuwa Wasafi muda mrefu ila Diamond hakumpenda hapo awali alimpenda Tanasha Donna, lakini Zuchu sasa hivi ni staa ndiyo Diamond anajifanya kapagawa,” mwingine alidakia.

Hii si mara ya kwanza kwa wasanii hao kuashiria wazi kwamba huenda ni wapenzi ila wanapoulizwa hadharani huwa wanakataa katakata na kusema ni kazi tu za kimuziki.

Wiki iliyopita wakati Diamond akiwa ziarani ziarani Ulaya, Zuchu alimfuata na kukutana naye kule Ufaransa ambapo haijulikani kipi kilichomchukua kule au ni kumfuata tu Diamond ambapo baadaye walionekana kwenye picha na video wakiwa katika mkao wa kuashiria huba limejaa ndoo hadi linamwagika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live