Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond atema madini ya kuingiza fedha kupitia mitandao

Diamond Atema Madini Ya Kuingiza Fedha Kupitia Mitandao Diamond atema madini ya kuingiza fedha kupitia mitandao

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akiwa kwenye jukwaa la Acces ambalo limefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajili ya kuwakutanisha wadau wanaofanya muziki, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ametoa siri kwamba, You Tube hailipi kivile.

Diamond ambaye alipata nafasi ya kutoa madini na kusikilizwa na mamia ya wadau wa muziki waliohudhuria, alisema wasanii wanatakiwa kuanza kujiongeza kwa kufanya jitihada za kujitangaza zaidi kwenye mitandao tofauti tofauti ambayo inalipa.

"Mfano You Tube, ukifikisha views milioni moja, unapata kama kiasi hicho hicho cha pesa lakini mtandao kama Spotfy, unapata streem milioni moja unapata kama dola 3000 karibu milioni saba hivi," alisema Diamond.

Diamond alisema, wasanii wa mataifa mengine walishapiga hatua kwenye mitandao kama hiyo hivyo ni wakati wa wasanii wazawa kufanya jitihada hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live