Dar es Salaam. Mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz ameahidi kumdhamini mwanafunzi mmoja wa Shule ya Sekondari Rugambwa atakayefanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2019.
Amesema mwanafunzi huyo atapata uidhamini wa kuendelea na masomo nchini Uingereza au Marekani.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Julai 19, 2019 baada ya mwanamuziki huyo na timu itakayoshiriki tamasha la Wasafi Festival kuitembelea shule hiyo iliyopo mkoani Kagera, Tanzania.
Diamond amesisitiza kuwa ni yule atakayefaulu kwa kiwango cha juu katika mtihani huo.
Mkali huyo wa Bongo Fleva amesema atazungumza na uongozi wa shule hiyo ili kupanga mikakati ya kufanikisha jambo hilo.
Diamond amesema atazungumza na wadhamini wake katika tamasha la Wasafi ambao ni Global Education Link kwa ajili ya kupata nafasi moja ya ufadhili.
Pia Soma
- Uganda watua Tanzania kujifunza usajili wa vizazi, vifo
- CRDB yatoa Sh150 milioni kufanikisha mkutano wa ALAT
- Seneta aagiza app ya FaceApp ichunguzwe
- Tanzania kuandaa kongamano la biashara la Tanzania-Uganda
“Kwa mtu anayefanya vizuri katika masomo nitampa udhamini wa kwenda kusoma Uingereza au Marekani na hii kwa msaada wa chuo cha Global Education Link nitawaomba wanipatie nafasi ya mtu mmoja wa kwenda kusoma huko,” amesema Diamond.
Global Education Link ni taasisi inayojishughulisha na uwakala wa wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya nchi.