Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond atangaza kuwa mtayarishaji mkuu albamu ya Barnaba

Barnaba Na Diamond Diamond atangaza kuwa mtayarishaji mkuu albamu ya Barnaba

Mon, 15 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mashabiki wa burudani wanafahamu kwamba mwanamuziki Barnaba anakwenda kuzindua albamu yake iitwayo Love Sounds Different lakini habari tu ikufikie kwamba Diamond Platnumz ndiye mtayarishaji Mkuu wa albamu hiyo.

Hilo limebainika juzikati pande za Sauz wakati Diamond Platnumz alipokuwa anamtambulisha Barnaba kwa Rapa Focalistic.

Kupitia ukurasa wa Wasafi, wameshea kipande cha video kinachomuonesha Diamond akifanya zoezi la utambulisho na kusindikiza na ujumbe huu:

“Moment ndani ya Afrika ya Kusini ????????, @diamondplatnumz akimtambulisha @focalistic kwa MOPOA @barnabaclassic. @diamondplatnumz amemueleza Foculist kuwa @barnabaclassic ndio Mwanamziki aliye-inspire wanamuziki Wengi wa kizazi cha Sasa Tanzania ????????.

“Lakini Pia @diamondplatnumz amethibitisha kuwa Mtayarishaji Mkuu wa Album ya #LoveSoundsDifferent ya @barnabaclassic ambayo itazinduliwa AUGUST 16 , MLIMANI CITY!”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live