Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond atangaza balaa zito Wasafi Festival 2023

Diamond Tress Diamond Platnumz.

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mtendaji wa Wasafi Media, Naseeb Abdul Jumaa 'Diamond Platnumz' ameatangaza rasmi kuanza kwa Tamasha la Wasafi Festival 2023 ambalo limepewa kauli mbiu ya 'Hiyo imeenda'.

Akitangaza uzinduzi wa Tamasha hilo la Burudani, Diamond amesema kuwa baada ya kutofanyika kwa miaka mitatu, sasa wanakuja na ubunifu wa aina yake ambapo litaanza na utambulisho wa wasanii watakaokiwasha mikoa yote 10 ambayo Wasafi festival itafika.

"Leo tumewaita kwa ajili ya kuwakutanisha Watanzania katika Tamasha letu la Wasafi Festival ambalo hatujalifanya kwa muda mrefu, sasa tutalifanya mwaka huu.

"Mara ya mwisho tuliliifanya mwaka 2019, tukasimama, lengo letu ilikuwa tukifanya tena tufanye kitu kukibwa zaidi ya kile tulichofanya awali.

"Wasafi Festival yam waka huu itakwenda katika mikoa 10 ambayo tutaitaja baadaye. Hatufanyi tamasha tu kama tamasha, haileti maana, tunafanya kwa mambo makuu matatu ikiwa ni pamoja na kuburudisha, kuwaelimisha na kuwaonyesha fursa za kibiashara.

"Kwenye burudani hapo sihitaji hata kuzungumza, kuanzia mimi mwenyewe Mkurugenzi, wasanii wangu na wasanii wengine wengi katika kila aina ambao tutawaleta, niseme burudani haielezeki. Sio muziki tu, kutakuwa na waigizaji, vinyago, acrobatic na Sanaa nyingine nyingi.

"Leo tuna launch na kutangaza logo, Jumamosi ya Agosti 12, 2023 pale CCM Kirumba Mwanza tutafanya usajili wa wasanii na kutangaza orodha ya wasanii wote watakaokiwasha kwenye Wasafi Festival 2023 katika mikoa yote.

"Mkoa tutakaoanza nao kufanya Tamasha hili ni mkoa wa Mtwara kwa sababu ndiyo mkoa wa kwanza ambao tulianza kufanya Tamasha hili kwa mara ya kwanza, na sijafika kule muda muda mrefu.

"Pia, ni mkoa ambao ambao nimeanza kufanya shoo yangu ya kwanza tangu niwe msanii, isitoshe ndio mkoa ambao ulitoa msanii wa kwanza kujiunga na WCB wakati tunaianzisha, hivyo ni kama nyumbani licha ya mimi asili yangu kuwa Kigoma na Morogoro.

"Tamasha la kwanza litakuwa Septemba 2, 2023, balaa linaanzia Nangwanda Sijaona pale Mtwara. Tukitoka pale mkoa unaofuata ni Lindi pale Ruangwa, mkoa unaofuata ni Ruvuma, tutafanyia Songea. Kiingiulio kitakuwa si chini ya sth 10,000 kwa kila Tamasha, tutawatangazia.

"Tutafanya shoo za uhakika sio za kurukaruka, sio kila msanii ana sifa ya kupanda kwenye jukwaa la Wasafi Festival, lazima awe na ubora na uwezo mkubwa wa kufanya muziki na kufanya shoo, mtu akipanda akafanya mambo ya hovyo maana yake ametuvunjia heshima," amesema Diamond.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live