Dar es Salaam. Msanii maarufu Tanzania, Diamond Platnumz amesema anakwepa kufanya shoo Dar es Salaam mara kwa mara kwa sababu akiharibu atakuwa ameharibu kote.
Diamond amesema hayo leo Jumannen Juni 25, 2019 alipokuwa akizungumzia tamasha la Wasafi linalotarajia kuanza Julai 12,2019.
Amesema Dar es Salaam kila mmoja anajua kuimba, kucheza na ni msanii hivyo akitaka kufanya shoo lazima ajipange sana, ndiyo maana hafanyi kila mara.
"Siwezi kukurupuka kufanya shoo Dar, nikiharibu nitakuwa nimeharibu nchi nzima. Sasa ninajipanga na nitafanya kitu kikubwa hivi karibuni,” amesema Diamond ambaye mara ya mwisho kufanya shoo Dar es Salaam ilikuwa mwaka 2017