Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond asimulia alivyofeli mtihani THT

FB IMG Diamond Tht Diamond asimulia alivyofeli mtihani THT

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Big boss wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesimulia jinsi alivyohangaika kutafuta mlango wa kutokea na kujikuta akifeli mtihani katika Jumba la Vipaji Tanzania (THT).

Diamond amesimulia ishu hiyo usiku wa kuamkia Agosti 17, 2022 alipokuwa anatoa hotuba yake katika uzinduzi wa albamu ya Elius Barnaba ya Love Sound Different iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.

“Nakumbuka wakati huo nilikwenda pale THT na hasa niliamini nikionana na Barnaba basi nitakuwa nimetoboa. Lakini bahati mbaya sikuonana naye, nikafanyiwa mtihani nikafeli,” alisema Diamond.

Diamond alisema, mara baada ya kufeli hakukata tamaa, alimsaka Barnaba hadi kufanikiwa kumpata akampa ushauri wa kubadili baadhi ya mistari katika wimbo wake wa Kamwambie.

Alisema, alitamani sana wimbo huo amshirikishe Barnaba akiamini ndio utatoboa lakini hata hivyo Bob Juniour (prudyuza na msanii) akamwambia wauachie wimbo huo kwani si rahisi kumpata Barnaba.

“Nilimkatalia sana Bob Junior lakini ikafika wakati nikakubali na ndio kumbe Mungu ndio alikuwa anasema pengine fanya peke yako pengine ningefanya na Barnaba na jinsi anavyojua angeweza kunifunika,” alisema Diamond.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live