Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ashindwa kujizuia akiwaaga watoto wake

Diamond Tiffah Mk(1) Diamond ashindwa kujizuia akiwaaga watoto wake

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ziara ya watoto wa supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambao ni Tiffah Dangote na Prince Nillan nchini Tanzania imemalizika siku ya Jumanne.

Staa huyo wa Bongo aliwasindikiza wanae hao hadi uwanja wa ndege walipokuwa wakirejea kwa mama yao, Zari Hassan nchini Afrika Kusini ambapo video zao kipindi cha kuagana zimeonyesha wakiwa kwenye hisia katika uwanja wa ndege.

Katika video hizo, bosi huyo wa WCB alionekana akiwakumbatia wanawe kabla ya kuwapungia mkono wa kuwaaga. Binti yake, Tiffah hakuonekana kuwa tayari kumuacha na hata alilia huku akimpungia mkono wa kumuaga.

"Tutaonana, nakupenda, ni sawa, nitakuja, nitakuja," Diamond alimwambia binti yake huku akimuaga kwaheri.

Yeye pia alionekana kuzidiwa na hisia huku akiondoka katika eneo la kuwaaga abiria la uwanja huo wa ndege.

Tiffah na Nillan walitua Tanzania Ijumaa wiki iliyopita na kupokelewa kwa furaha na baba yao Diamond kwenye uwanja wa ndege. Inaaminika kuwa dhumuni la ziara hiyo ilikuwa ili wapate kusherehekea Eid pamoja na mzazi huyo wao na familia yake nyumbani kwake katika jiji la Dar es Salam.

Mama yao, mwanasosholaiti Zari Hassan, ambaye hivi majuzi tu alifunga ndoa (Nikah) na mchumba wake Shakib Cham Lutaaya, hata hivyo hakufuatana nao katika ziara hiyo, kama ilivyokuwa katika siku za nyuma.

Wakati akiwapeleka nyumbani baada ya kuwalaki Ijumaa usiku, Diamond alionekana kufurahi sana kuwaona tena. Huku akirekodi tukio hilo, aliwaomba wanawe wawasalimie Watanzania na kuwajulisha kuhusu ziara yao.

"Babaa (Nillan). Isalimie kamera. Sema hello Tanzania, tuko hapa kutoka Afrika Kusini," Diamond aliwaambia huku wakirudia maneno yake.

Aliendelea kusema, "Tiffah yuko hapa. Unaendeleaje kipenzi (Tiffah)," huku akimuonyeha binti yake kwenye kamera.

Tiffah na Nillan hata hivyo hawakuonekana wachangamfu, labda kutokana na uchovu wa safari ya kutoka Afrika Kusini hadi Tz.

Huku watoto wake wakiwa wamesafiri kuenda Tanzania, Zari Hassan na mumewe mwenye umri wa miaka 31 walishiriki muda pamoja na kujivinjari katika sehemu mbalimbali za burudani nchini Afrika Kusini.

Wawili hao ambao pia walikuwa pamoja na marafiki wengine walinasa baadhi ya kumbukumbu nzuri kwenye kamera.

Katika moja ya video alizochapisha, Zari alisikika akisifia mwonekano wa mpenzi huyo wake mdogo kwa umri. "Usiku wetu, mpenzi unakaa vizuri," Zari alimwambia Shakib.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live