Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ashinda tuzo Nigeria, awabwaga Harmonize na Zuchu

FB IMG Diamond Tht Diamond

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diamond ameshinda katika kipengele cha Msanii Bora Afrika Mashariki baada ya kuwabwaga Harmonize, Zuchu, Meddy (Rwanda), Eddy Kenzo (Uganda) na Nikita Kering (Kenya).

Hata hivyo, Diamond ameshindwa kufua dafu kwenye kipengle cha Msanii Bora wa Mwaka Afrika ambacho alikuwa anawania na Black Coffee, Davido, Soolking, Aya Nakamura, Wizkid na Burna Boy ambaye ameibuka mshindi katika tuzo hizo zinazoandaliwa nchini Nigeria.

Msanii wa Nigeria, Wizkid ndiye ameondoka na tuzo nyingi zaidi akishinda vipengele vya Wimbo Bora wa R&B (Essence ft. Tems), Wimbo Bora wa Kushirikiana (Essence ft. Tems), Wimbo Bora wa Mwaka (Essence ft. Tems), Albamu Bora ya Mwaka (Made In Lagos)  na Albamu Bora ya Afrobeats (Made In Lagos).

Wasanii wengine waliofanya vizuri ni Burna Boy akishinda tuzo mbili, Davido tuzo mbili, huku Tems, Innoss'B, FireBoy DML, Patoranking, Mr. Flavour, Fave, Latifa, D'Banj na wengineo wakishinda tuzo moja moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live