Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ashika namba 5 Afrika

FB IMG Diamond Tht Diamond ashika namba 5 Afrika

Fri, 23 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameshika namba 5 barani Afrika kwa kuwa na wafuasi milioni 7.1 kwenye mtandao wa Youtube.

Pia anashika nafasi ya kwanza kwa kuwa wafuasi wengi zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Afrika Kusini.

Katika orodha hiyo, nafasi ya kwanza inashikwa na msanii Mohamed Ramadan kutoka nchini Misri akiwa na wafuasi milioni 14.2 na kufuatiwa na msanii Saad Lamjerred kutoka Morocco ambaye ana wafuasi milioni 14 Youtube.

Soolking msanii kutoka Aalgeria anashika nafasi ya tatu katika orodha hiyo akiwa na wafuasi milioni 9.5 huku namba nne ikishikwa na Tamer Hosny kutoka nchini Misri akiwa na wafuasi milioni 7.77.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live