Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ashauri wimbo wa Enjoy 'ufutwe'

Diamond X Jux Diamond ashauri wimbo wa Enjoy 'ufutwe'

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amemshauri Jux kutumia uungwana kuufuta wimbo wa Enjoy kutokana na jinsi ulivyopokelewa huku akisema kuwa video ya wimbo huo anaiyona Trending namba moja hadi 2030.

Diamond ametoa maoni hayo kwenye ukurasa wa Instagram mara baada ya Jux kuwashukuru mashabiki kwa mapokeo ya wimbo huo mpya aliomshirikisha Diamond ambayo yameifanya ngoma hiyo kushika namba moja trending huko YouTube.

Jux aliandika hivi;

"SHUKHURANI ZETU ZA DHATI ZIWAFIKIE MASHABIKI WETU WOTE WANAOUPIGANIA MZIKI WETU MZURI ❤️ MNATUTIA NGUVU SANA! ASANTENI NA TUNAWAPENDA"

Diamond ndipo akakomenti hivi:

"Kwa Support na Upendo Huu mkubwa tunaoupata, mi naona labda tutumie uungwana tuidelete (tuufute) tu Nyimbo…maana Nikiwaza na Video inakuja basi naona Trend itakua hadi Mwaka 2030."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live