Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond arejesha tabasamu la Hawa ‘Nitarejea’

70522 Hawa+pic

Fri, 9 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii Diamond Platnumz amezidi kurejesha tabasamu kwa msanii Hawa Said maarufu Hawa Nitarejea  baada ya kupanda naye jukwaani mkoani Dodoma na kuimba wimbo aliomshirikisha wa ‘Nitarejea’.

Diamond anafanya hivyo ikiwa imepita takribani miezi kumi tangu alipomsaidia Hawa matibabu kwa kumpeleka nchini India baada ya msanii huyo kusumbuliwa na maradhi ya tumbo, baadaye kubainika kuwa alikuwa na tatizo la moyo.

Mbali na kuimba pamoja jukwaani, Hawa pia ametoa wimbo ‘Nacheka’ huku akilieleza Mwananchi kuwa wimbo huo ni zawadi kwa mashabiki wake.

Katika wimbo wake huo, Hawa ameeleza nyakati alizopitia, hasa wakati alipokuwa mgonjwa na kuwashukuru wote waliomsaidia mpaka amepona.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz