Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond aongoza kwenye chart Nigeria baada ya miezi 7

Diamond Mtv Diamond aongoza kwenye chart Nigeria baada ya miezi 7

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wimbo wa Diamond Platnumz kutoka Tanzania – My Baby – aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria, Chike kwa mara nyingine tena umerudi kwenye kilele cha chart za muziki nchini Nigeria.

Hii ni baada ya miezi saba baada ya kuachia kolabo hiyo ya nguvu iliyotamalaki kitakwimu katika majukwaa mbalimbali ya kidijitali ya kupakua miziki.

Dimond Platnumz mwenyewe alithibitisha habari hizi kupitia kwa Insta story yake akionesha kutamba kuwa wimbo wake hata baada ya kutoka miezi 7 iliyopita na kuonekana kama umesahaulika katika ulimwengu wa sasa ambapo mambo yanakwenda kwa kasi na kusahaulika kwa haraka, wimbo wake bado unazidi kufufuka.

Kwa kifupi, wimbo huo unaweza ukatafsiriwa kama kifaurongo ambaye anayeyuka na kudhaniwa amekufa na kusahaulika lakini anawashangaza wengi kwa kufufuka tena na kurudi katika nafasi yake ya awali.

Tangu alipoachilia video ya wimbo huo miezi 7 iliyopita, katika mtandao wa YouTube, My Baby una watazamaji Zaidi ya milioni 18.

Wimbo huo ni wa kimapenzi na baadhi ya watu wanahisi kwamba umefufuka ghafla na kurudi katika nafasi ya kwanza nchini Nigeria mwezi huu wa Februari kutokana na sikukuu ya wapendanao - Valentines Day - ambayo watu wengi hutumia nyimbo za kimapenzi kuwaimbia na kuwatumia wapenzi wao kama ishara ya kuonesha kujituma kwao kimapenzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live