Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond anatumia milioni 6 kusuka nywele zake

Diamond Kusuka Diamond anatumia milioni 6 kusuka nywele zake

Sat, 24 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lisma, ambaye ni msusi wa wasanii alisema Diamond huwa anatumia kiasi cha Tsh milioni 6 kwa mwezi.

Sasa taarifa mpya imeibuka kuhusu yule mtu ambaye anashughulika kupendezesha kichwa cha msanii namba moja wa muda wote Afrika Mashariki, Diamond Platnumz.

Inaarifiwa kwamba mitindo ya usukaji wa Diamond Platnumz ni kazi ya mikono ya mwanadada mmoja mwenye saluni maarufu kwa jina Lisma.

Diamond ni msanii ambaye mara kwa mara anaonekana kubadilisha mitindo ya ususi kichwani mwake na kazi hiyo hufanywa na mwanadada Lisma.

Katika mahojiano, Lisma alifichua kuwa msanii Diamond husuka mara mbili kwa mwezi na kila mara anapotembelea saluni yake basi huwa anaacha kiasi cha Tsh milioni 6 (yaani Tsh milioni 3 mara mbili kwa mwezi) kwa ajili ya kusuka na kusuka nywele zake.

Mwanadada huyo si tu msusi wa msanii Diamond bali pia anawashughulikia mastaa mbali mbali, wake kwa waume nchini humo na kufanya mionekano ya vichwa vyao kuvutia kwa mashabiki.

Lisma ndiye msusi wa mastaa mbali mbali kama vile aliyekuwa mpenzi wa Diamond Wema Sepetu, aliyekuwa mpenzi wa Rayvanny, Fahyvanny, msanii wa kike ndani ya WCB Zuchu, miongoni mwa majina mengine tajika nchini humo.

Watu mbali mbali wamekuwa wakimsifia msanii Diamond Paltnumz kwamba si mchoyo katika kumwaga mihela.

Chawa wake Issa Azam mara kadhaa amenukuliwa akimsifia pakubwa kwamba msanii huyo amebadilisha maisha ya watu wengi na hata akasikika akisema kwamab ikatokea amefariki dunia leo basi atakayemzika awe ni Platnumz na wala si ndugu zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live