Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond anamdhalilisha Zuchu

Zuchu Amsifia Diamond, Asema Ni Daraja La Mafanikio Ya Wasanii Wengi.png Diamond anamdhalilisha Zuchu

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitendo alichokifanya Diamond kwa Zuchu kumshika chuchu zake hadharani mbele ya umati ni udhalilishaji kwa wanawake.

Maskini Zuchu baada ya kushikwa hapo, aliona aibu akainama kidogo huku Diamond na Mashabiki wakibakia kuchekelea.

Zuchu hapendi kufanywa hivyo hata kama ni mapenzi yanahitaji faragha. Tunahitaji kuungana kama watanzania kupinga unyanyasaji huu wa kijinsia.

Zuchu anajua kuwa Maisha yake bila Mondi hatoboi ndiyo maana anafanyiwa yote lakini atafanya nini?

Ni kama mtoto yatima asiye na sauti

Niliumia sana baada ya kuona Diamond akimfanyia hicho kitendo.

Katika sehemu nyeti za mwanamke ambazo mwanaume hutakiwi kumshika hadharani mojawapo ni Mawaziwa ( chuchu) makalio pamoja na katikati ya miguu.

Simkatazi Diamond kushika sehemu hiyo, ashike hata mwaka mzima kila siku lakini iwe faragha. Amuheshimu mtoto wa mzazi mwenziye.

Je atajisikiaje kama siku moja ataona mwanaye akifanyiwa hivyo?

Unadhani alichofanyiwa Zuchu ni sawa?

Je ataacha lini kumnyanyasa?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live