Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ana uwezo wa kuwasaidia wasanii wa Bongo kutoboa nje, hajaamua tu!

Diamondz.jpeg Diamond Platnumz

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Neno kupeperusha Bendera ya Taifa” ni pana kidogo, Sanaa haihitaji mtu mmoja pekee kujulikana nje ya mipaka ya Tanzania, tunahitaji kuwa nao wengi, ila kabla hatujawanyoshea vidole wasanii hawa ambao wanalitafuta soko la Kimataifa.

Hivi huyu mmoja mwenye matamanio ya kuona hata akifa leo bado bendera ya Tanzania itabaki kwenye list ya wasanii 10 Afrika wenye ushawishi duniani, anafanya jitihada gani kwa wasanii wenzie?.

Najua utimu unamaliza sana tasnia ya muziki, alafu tunajiroga wenyewe na kuhitisha mikutano ya kutafuta wachawi wa hii sanaa, kumsaini mtu kwenye Label si msaada na haitoshi kusema umesaidia.

Si kila msaada lazima ukurudishie malipo. Tunamsema Diamond, maana ndiye msanii pekee toka Bongo ambaye kwa sasa ana mabawa ya kupaa umbali mrefu zaidi nje ya mipaka ya Bongo kuliko wasanii wengine.

Tunakumbuka alicho kifanya Burna Boy kwa Rema, Ruger na Omahlay, mwezi Agosti 2021, kuwabeba toka Nigeria na kuwapandisha kwenye show yake kwa mara ya kwanza pale O2 Arena Uingereza, Diamond anashindwa nini kumshtua Marioo ajiandae maana anaenda kumpandisha kwenye jukwaa la Afronation.

Kwa nini Maluma aliweza kumpandisha Rayvanny kwenye majukwaa makubwa mara 3, kwani alishindwa Mama Tetema kuimba mwenyewe? By the way Marioo ni mfano tu ila tuna wasanii wengi ambao naamini kama outsiders watawajua basi itakuwa ni hatua kubwa sana kwao.

Tukitoka nje tunarudi home kujiliza kama Romy Jons, kwa nini tuna msanii mmoja kimataifa, Ni Unafiki mkubwa, Diamond ana uwezo wa kuwasaidia wenzie kwa njia hii ila ukweli ni kuwa Bongo kuna umimi.

Sio muziki tu, sehemu nyingi watu wanaminyiana nafasi kitu ambacho si mchongo. Alafu utasikia shabiki wa mchongo anakwambia kwani yeye alisaidiwa na nani? Hatuwezi kuwa sawa, ma-gap lazima yawepo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live