Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond amuomba radhi mwanaye kwa kutohudhuria bethidei yake

Diamond Amuomba Radhi Mwanaye Kwa Kutohudhuria Bethidei Yake Diamond amuomba radhi mwanaye kwa kutohudhuria bethidei yake

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz amemtuliza mwanawe Prince Nillan baada ya kushindwa kuhudhuria sherehe ya siku yake ya kuzaliwa mnamo Jumatano, Desemba 6.

Katika taarifa yake siku ya Alhamisi, bosi huyo wa lebo ya WCB alimtaka mtoto huyo wake wa pili wa mwanasosholaiti Zari Hassan asiwe na wasiwasi kuhusu yeye kutohudhuria sherehe yake kwani anapanga kulipa fidia.

Alisema ili kulipia kukosa karamu zilizopita, atawaandalia tafrija kubwa kijana wa miaka saba na dada yake mkubwa Tiffah Dangote.

“Nimekosa siku yako maalum na ya dada yako mwaka huu mwanangu.. Ila usijali, nitawafanyia wote Birthday Party maalum kwa ajili yako na dada yako mtakapokuja kwa ajili ya mkesha wa mwaka mpya nchini Tanzania!!!,” Diamond alisema kupitia Instagram.

Staa huyo wa bongo fleva aliendelea kumhakikisha mwanaye na Zari kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

"Kumbuka Papa anakupenda sana @princenillan," alisema na kuambatanisha taarifa yake na picha ya mvulana huyo wa miaka saba.

Prince Nillan aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya saba siku ya Jumatano huku dada yake Tiffah Dangote akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 8 mnamo Agosti 6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live