Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond amtupia dongo Harmo: Range ni kwa ajili ya warembo tu!

Zuchu Mondi03 Diamond amtupia dongo Harmo: Range ni kwa ajili ya warembo tu!

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametupa dongo kwa hasimu wake, Harmonize akidai kuwa magari aina ya Range Rover ni kwa ajili ya wanawake tu na si wanaume kama ambavyo amekuwa akitamba.

Kupitia Insta story yake @diamondplatnumz ameandiki ujumbe huo akipeleka kwa msanii wake, @officialzuchu baada ya kununua gari aina ya Range Rover.

@diamondplatnumz amemueleza @officialzuchu namna anavyomfanya ajivunie yeye na kutembea kifua mbele.

Pia @diamondplatnumz amesema kuwa anaomba kurasimisha kuwa Range ni Gari maalumu kwa ajili ya Queens wote.

Kauli hiyo ya Diamond inakuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Harmonize atangqze kuwa kwa msanii yoyote wa Bongo ambaye hamiliki Range basi afute namba yake kwenye simu yake na asiwasiliane naye tena.

Unaonaje hii vita, itamwacha mtu salama?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live