Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ampongeza Zuchu Sukari kugonga views milioni 100

Mama Diamond Akanusha Penzi La Mwanaye Na Zuchu 'sio Wapenzi'.png Diamond ampongeza Zuchu Sukari kugonga views milioni 100

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa muziki Africa, Diamond Platnumz amempongeza msanii wake Zuchu kwa kuweka historia ya kuwa msanii wa kwanza wa kike kutoka Afrika Mashariki kuwa na video yenye views zaidi ya milioni 100.

Hii ni baada ya ngoma ya Zuchu #Sukari ambayo hajamshirikisha mtu yeyote, kugonga views milioni 100 kwenye platform ya YouTube.

"Ukiona kwa macho ni kama jambo la kawaida, ila sasa unapojaribu kufanya ndio unajua uzito wake!! Sukari: by female artist 100% Swahili song!, no feature! 100m viewers! ni heshima kubwa kwa @wcb_wasafi, music industry na nchi," ameandika Diamond Platnumz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live