Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ampongeza Ruto kwa kushinda Urais wa Kenya

Odinga Mondi Diamond ampongeza Ruto kwa kushinda Urais wa Kenya

Tue, 16 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongofleva toka WCB Wasafi, Diamond Platnumz amempongeza William Ruto (55) kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya na kusisitiza huo ni muda wa kuijenga nchi hiyo.

Mda mfupi uliopita Tume ya Uchaguzi Huru na Mipaka (IEBC) imemtangaza aliyekuwa Naibu Rais, William Ruto (55) kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano kwa tiketi ya Chama cha UDA kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 9, 2022.

"Pongezi sana Wana Kenya kwa kuhitimisha zoezi la Uchaguzi na kumpata Rais leo. Sasa hivi si team Ruto, Wajackoyah, ama team Odinga, ni pamoja team Kenya" amesema Diamond.

Utakumbuka Tume imesema Ruto amepata Kura 7,176,141 sawa na asilimia 50.49 huku akifuatiwa na Raila Odinga kutoka Chama cha Azimio la Umoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live