Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ampa ujumbe mzito bintiye Tiffah

TIFFAH DANGOTE Diamond ampa ujumbe mzito bintiye Tiffah

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukiachana na shughuli kuwa ya bethidei kuwa ya kitaifa kule Sauz, Diamond amempa ujumbe mzito binti yake Tiffah ambaye alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Diamond alisema, anamuombea kwa Mungu binti yake huyo awe na akili ili aweze kufanikiwa maishani na kumlea yeye pamoja na ndugu zake.

“Mwanangu Latiffah nakupenda sana, sina kikubwa cha kukupa zaidi ya hichi kidogo ninachokipata, nikusomeshe ukue, ukawe msaada. Unisaidie mimi baba yako, mama na bibi yako,” alisema Diamond.

Tiffah afanyiwa bonge la pati la bethidei Agosti 7, 2022 la kutimiza miaka 7 pande za Sauz ambapo Diamond alikuwa na timu nzima ya Wasafi ikiwemo familia yake, mama Diamond na Esma Platnumz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live