Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ampa kiwanja Diva

Diva Na Mondi.jpeg Diamond ampa kiwanja Diva

Sat, 26 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diamond Platnumz ni Mkurugenzi Wa Wasafi Media huku Zuchu akiwa ni msanii wake; kwa pamoja wamemfanyia kufuru mtangazaji Diva kwenye tukio la sherehe yake ya ndoa na Abdul.

Katika tukio hilo lililochukua nafasi katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar usiku wa kuamkia leo Machi 26, 2022, mbali na kutumbuiza pia wamemjaza manoti na mijizawadi kedekede.

Diamond au Mondi amemuongezea mshahara kwa asilimia 50 kisha amempa kiwanja (Beach Plot) kilichopo Kigamboni Square Meter 2000 na pesa taslimu shilingi milioni 10 pamoja na simu mbili za kisasa na na TV.

Kwa upande wake Zuchu; kama Balozi wa Utalii Zanzibar ameahidi kugharamia safari pamoja na bata zima pale Diva na Abdul watakapokwenda Zanzibar kwa ajili ya fungate.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live