Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond amkabidhi Jackline kwa Zuchu

Diamond Amkabidhi Jackline Kwa Zuchu Diamond amkabidhi Jackline kwa Zuchu

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ameendelea kuigusa jamii baada ya leo kumuhakikishia mrembo Jackline (aliyepata ulemavu kwenye ajali) kuwa atahakikisha anapata kolabo na Staa wa Bongo Fleva, Zuhura Othuman 'Zuchu' ili kukuza kipaji chake na jina.

Jackline ambaye amefika kwenye kipindi cha Mashamsham kuomba msaada kwa Watanzania amepata dili hilo baada ya kusema kuwa mbali na kutaka msaada wa matibabu pamoja na elimu, pia ana kipaji cha kuimba ambacho angependa kukiendeleza.

Ahadi ya Diamond Platnumz imeelezwa na Steve Nyerere wakati wa mahojiano maalum kwenye kipindi cha Mashamsham.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live