Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ametuzidi, ni mkubwa, tukubaliane na hilo-H Baba

Noel Mwanamitindo Diamond ametuzidi, ni mkubwa, tukubaliane na hilo-H Baba

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa Bongo Fleva, Hamis Ramadhani ‘H Baba’ amefunguka kuwa, supastaa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewazidi wasanii wengi Bongo hivyo hakuna budi kukubaliana na ukwlei huo.

H Baba ameyasema hayo alipopigwa simu na Kipindi cha The Switch cha Wasafi FM, ambapo alieleza kuhusu ishu ya Diamond kumuambia kuwa ajiandae wafanye ngoma ya pamoja baada ya kufanya na Baba Levo.

“Kolabo yangu mimi na Nasibu itakuwa saparizi. Diamond ni mtu wa watu kaniambia huu ni muda wako naomba ufanye maandalizi sababu namhitaji yule H Baba wa Poteza. Ngoma ambayo Diamond kafanya na Baba Levo ni kali sana.

“Baba Levo ataachia ngoma mbili, moja kafanya na Diamond na ndio sababu ya kuniambia na mimi niandae ngoma. Kitu ninachokiona kwenye huu muziki, usimdharau aliyekuzidi, Diamond ni mkubwa,” alisema H Baba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live