Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ametusaliti Bongo - mdau

Diamondplatnumz 1695285087238.jpeg Diamond ametusaliti Bongo - mdau

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa miaka mingi sana tumekuwa tukimtazama sana Diamond Platnumz kuwa ndio msanii pekee mwenye mabavu ya kuufanya mziki wetu kufika kimataifa imekuwa tofauti na mtazamo yetu.

Siku za hivi karibuni Diamond amekuwa msanii wa kisujudia radha ya mziki wa Amapiano na kuitupa mbali Bongo Fleva, kwa muktadha huo inamaanisha Diamond ameamua kutusaliti sisi Watanzania na kupromote mziki wa Madiba "Amapiano".

Msanii kama Asake wa Nigeria hakutaka kabisa kupoteza Identity ya Afrobeat, aliamua kuchanganya Amapiano na Afrobeat "Afropiano" bila kiathiri vionjo ya mziki wa nchini mwao, ila tumaini letu amekuwa mstari wa mbele kabisa kuua mziki wetu.

Kwa sasa Diamond ameanza kupoteza mvuto kabisa kwenye tasni hii ya Bongo Fleva ndio maana ameanza kijiwekeza kwenye vitimbwi vya Nje ya mziki. Kwa Upande wangu Kwa sasa Nedy Music ni msanii mkali kuliko Diamond Platnumz.

Amesema mdau wa muziki (jina kapuni).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live