Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond alitaka kumfunga Mwijaku akachutama, kwa Mpoki anakwama wapi?

Maxresdefault   2022 12 01T100624 Diamond alitaka kumfunga Mwijaku akachutama, kwa Mpoki anakwama wapi?

Fri, 2 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mtoto Nasib Jr wa Diamond na Tanasha amezaliwa, mtangazaji wa Clouds Media, Burton Mwemba 'Mwijaku' alijitoa ufahamu akaanza kutangaza kwamba toto huyo ni wake, jambo lililoibua sintofahamu.

Kilichofata baada ya hapo mwanasheria wa Diamond alimuita Mwijaku, akamweleza kuwa iwapo ana uthibitisho huyo mtoto ni wake basi atautoa Mahakamani, lakini akishindwa tu basi Diamond atamfunga.

Kutokana na sakata hilo, baada ya kuona mambo ni mazito, Mwijaku aliamua kukiri kufanya kosa na anakamuomba msamaha Diamond na Tanasha.

Wadau wanasema, kama Diamond aliweza kumaliza sakata hilo la Nasib Jr wa Tanasha dhidi ya Mwijaku, je, anashindwa nini kwa sakata la Dylan wa Mobeto dhidi ya Mpoki. Je anafurahi kuona mtoto huyu kila siku akizushiwa baba mpya?

Sio kwamba Diamond haelewani na Mobetto, tunaona mara kibao mwanamke huyo anaalikwa kwenye matukio ya Wasafi, sasa kwa nini kwenye raha wanamualika lakini kwenye matatizo wanamtupa? Kuna siri gani hapa?

Hivi karibuni, Mpoki alisema kwa mafumbo kuwa mtoto wa msanii mmoja (Mobeto japo hakumtaka jina) ni wa msanii mwenzake aliyefunga ndoa hivi karibuni (Billnass) na si Diamond na kwamba Diamond ameshakata mrija wa kumpa matumizi mtoto huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live