Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Diamond alinifukuza Wasafi kisa Harmonize" - Sholey

Sholey Sholey

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza densi rasmi wa msanii Rayvanny, Sholey amefunguka kilichosababisha yeye kufukuzwa katika miradi ya video za msanii Diamond Platnumz ambaye pia ni CEO wa Lebo ya WCB.

Akizungumza, Sholey ambaye amekuwa akionekana kwenye video za wasanii wengi tu ndani na nje ya WCB Wasafi tangu mwanzo kama vixen alisema alishtukia ghafla ametemwa na Diamond.

Sholey amesema tangu awali amekuwa akicheza kwenye video za Diamond, Harmonize, Rayvanny na hata Lavalava, lakini kitendo cha kutemwa kwenye video za Mondi bila kujuzwa sababu ilihujumu nafsi yake sana mpaka kujihisi kukosa amani kuendelea kuwepo pale.

Alisema kwamba alihisi kutemwa kwake kulikuja pindi tu baada ya kuonekana kwenye wimbo wa Harmonize, Ushamba, wimbo ambao msanii huyo aliutoa muda mrefu tu baada ya kuondoka Wasafi kwa shari.

Ila alisisitiza kwamba yeye kucheza kwenye wimbo wa Harmonize hakukuwa tatizo kwa sababu hakuwa na mkataba ndani ya Wasafi ulikuwa unamwekea mipaka ya wasanii wa kufanya kazi nao na wale wa kutofanya kazi nao.

“Nilijikuta tu nimetolewa kwenye kazi za Diamond. Mimi nilihisi ni kwa sababu ya kutokea kwenye wimbo wa Harmonize ‘Ushamba’ mimi ni mcheza densi tambua, nafanya kazi popote. Diamond hakuniambia kwamba Sholey naomba usicheze kwa mtu yeyote,” alisema vixen huyo.

Sholey alielezea kwamba wapambe wa Diamond ndio walimwambia atoke kwenye wimbo wa Diamond ambao alikuwa ashiriki kucheza kwa kile walichomtajia kwamba hana msimamo na ana tamaa ya kuonekana kote kote mpaka kwenye upande wa mahasidi wa Diamond zikiwemo video za Harmonize.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live