Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond alianza kuzikanyaga kapeti za BET kabla ya Burna Boy, kilichotokea...!

Diamond Burna Wizkid Diamond alianza kuzikanyaga kapeti za BET kabla ya Burna Boy, kilichotokea...!

Fri, 2 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diamond Platnumz ndiye msanii wa kwanza tokea Afrika Mashariki na hata mbele ya Burna Boy, kuwa nominated kwenye tuzo za BET, ambapo kwa mara ya kwanza alikuwa nominated kwenye tuzo hizo mwaka 2014 katika kipengere cha “Best International Act” na bahati mbaya kwake ni kuwa hakufanikiwa kubeba tuzo hiyo mbela ya Davido aliyeinyakua.

Ilimchukua mwaka mmoja tu kukaa kitaa kabla BET hawajamtaja tena Diamond kuwania kipengere hicho mwaka 2016, ikiwa ni mara yake ya pili, hakufanikiwa pia kuchukua tuzo hiyo mbele ya Black Coffee (Mshindi) tokea South Afrika.

Miaka 5 mbele (2021), Diamond anakuwa nominated tena kwa mara ya 3,anaambulia patupu mbele ya Burna Boy (mshindi).

Waswahili wanakwambia kuchelewa sio kufika, wakati Diamond anakanyaga Red Carpet ya BET mwaka 2014, Burna Boy anafanya shows za Kidimbwi pale Lagos nchini Nigeria, Miaka mitano mbele (2019), Burna Boy anakuwa mkubwa ndani na nje ya bara la Afrika kupitia Album yake ya African Giant, hasa projects zilizo ibeba Album hiyo, On the Low na Gbona, anaingia kwenye tuzo za BET kwa mara ya kwanza na kuibeba tuzo hiyo kwenye kipengere cha Best International Act.

Hakuishia hapo tu, akaibeba tena tuzo hiyo kwa miaka mingine miwili mbele mfululizo, 2020 na 2021 ambapo anakutana na Simba miaka 8 mbele kwenye tuzo hizo toka Diamond awe nominated kwa mara ya kwanza.

Kinacho wafananisha Diamond na Burna Boy kwenye BET, wote wamekuwa nominated mara 3, na kinacho watofautisha, Burna Boy kabeba tuzo hiyo kwenye nominations zake zote 3, wakati Diamond akikosa kwenye nominations zake zote 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live