Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond aliamsha upya na Zari

Zari Diamonmd Diamond aliamsha upya na Zari

Thu, 11 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zari The Boss Lady; ni mwanamama soshalaiti maarufu Afrika Mashariki ambaye ameweka wazi kinachoendelea kati yake na baby daddy wake, Diamond Platnumz wakidaiwa penzi lao limechipuka upyaa.

Zari anasema kuwa, anashirikiana vizuri na Diamond Platnumz katika malezi ya watoto wao wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan.

Zari anasema kuwa, yeye na Diamond wamekuwa wakijadiliana mara kwa mara kuhusu njia bora ya kuwalea watoto wao.

“Tumefanya malezi ya kushirikiana kuwa rahisi sana. Tumekuja pamoja na kusema tunataka bora zaidi kwa watoto wetu, tunaketi na kuongea,” anasema Zari.

“Tuna maslahi yao bora moyoni; wanataka nini? Wanataka kwenda wapi? Wanajiona wapi?"

Zari alikuwa akizungumza wakati wa pati kubwa iliyoandaliwa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya binti yao, Tiffah Dangote.

Zari anasema kuwa uhusiano wake na Diamond sasa umekuwa mkubwa zaidi ya wakati ambapo walikuwa kwenye mahusiano.

“Nadhani imekuwa rahisi kwa sababu sasa tunaelewana zaidi, siyo kama wapenzi lakini tunaelewana kama wazazi na marafiki. Mimi na Diamond kwa sasa hivi tumekuwa marafiki zaidi ya jinsi tulivyokuwa wapenzi. Inafanya mambo kuwa rahisi kwetu," anasema Zari; mama wa watoto watano.

Zari na Diamond walitengana mwaka wa 2018 baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa takriban miaka minne.

Licha ya kutengana kwao, wawili hao wameendelea kushirikiana vizuri katika malezi ya watoto wao wawili.

Diamond ameonekana mara nyingi akifanya ziara za kuenda Afrika Kusini kuwatembelea wanawe.

Wikendi iliyopita, Diamond na familia yake walijumuika na familia ya Zari kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Tiffah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live