Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond akutana na warembo wanaowania taji la ulimbwende wa Dunia

Diamond 4110 Diamond akutana na warembo wanaowania taji la ulimbwende wa Dunia

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul,’Diamond Platnum’ ametembelea na kuzungumza na washiriki wa shindano la dunia la Ulimbwende na Utanashati (Miss & Mister Deaf International ) kwa wenye changamoto ya kusikia “Viziwi” wakiwa katika hotel ya Peacock Jijini Dar es salaam.

Shindano hilo linalotarajia kufanyika tarehe 25 Novemba, 2023, katika ukumbi wa The Super Dome jijini Dar es Salaam. Diamond Platnnum ameahidi kulitangaza shindano hilo.

Diamond amepokelewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa Dk. Emmanuel Ishengoma pamoja na Katibu Mtendaji BASATA Dk.Kedmon Mapana na kutamburishwa washiriki hao.

Diamond Platnimz ameishukuru wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na BASATA na kuahidi kutoa vyombo vya habari vya WCB Kuhamasisha shindano hilo.

Aidha shindano hili linatarajia kufanyika tarehe 25 Novemba, 2023, katika ukumbi wa The Super Dome ulioko Masaki Jijini Dar es salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live