Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond akionekana na mrembo akiwa utupu

Zuchu Re (1) Diamond akionekana na mrembo akiwa utupu

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wamefurika mitandoani kumfariji Zuchu baada ya mpenzi wake Diamond Platnumz kuonekana na mrembo asiyetambulika wakiwa wamebarizi kwenye kochi.

Diamond alionekana anamshika shika makalio mrembo huyo ambaye alikuwa nusu uchi na kumlalia kifuani katika video hiyo ambayo imewagawanya wanamitandao.

Wengine walisema kwamba Zuchu hafai kuona video hiyo na kutaka msanii huyo asifikishiwe habari hizo, huku wengine bila huruma wakimtag kwenye chapisho hilo na kumcheka.

“Slide ya mwisho Zuchu hajaona,” mmoja alisema.

“Ila braza si vizuri unavyomfanyia Zuchu kwenye hiyo slide ya mwisho... kumbuka naye ana moyo wa nyama,” mwingine alidakia.

“Hiyo ya mwisho kuna mtu anaenda kuvunja vyombo uko leo ya mb zako,” mwingine alizua utani.

“Bro muda unaenda oa kaka”

Ikumbukwe hii si mara ya kwanza Diamond anaonekana kumkwaza Zuchu kwa makusudi kimapenzi baada ya wawili hao awali kuweka wazi kwamba walikuwa wanatoka kimapenzi licha ya kuwa na uhusiano wa Bosi na mfanyikazi.

Mwezi Mei baada ya kutoka kwa sehemu ya pili ya filamu ya uhalisia ya Netflix, Young Famous & African, Diamond alionekana akimla denda mwanasosholaiti kutoka Ghana, Fantana jambo ambalo lilimkwaza Zuchu.

Zuchu baada ya kuona kipande hicho wawili hao wakibusiana na hata Diamond mwenyewe kumsifia Fantana kwa ustadi wake katika kubusu, aliandika maneno ya kebehi yaliyolenga kwa bosi wake akisema;

“Mwambieni nilisema f***k you”.

Lakini pia itakumbukwa Zuchu mwenyewe aliweka wazi kwamba amemalizana kimahusiano na Diamond na uhusiano pekee uliosalia ni ule wa kufanya kazi chini ya lebo yake tu.

Diamond anaonekana na mrembo huyo asiyejulikana siku moja baada ya kupakia klipu iliyotoa sababu kwa nini amechagua maisha ya ukapera licha ya kuwa na kila kitu, lakini pia na watoto wanne kutoka kwa wanawake tofauti.

Kila mmoja sasa anasubiri kuona Zuchu atajibu nini kuhusu video hiyo ambayo imesambaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live