Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ajishangaa kukondeana ghafla

Diamond Kukonda Mn Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz

Tue, 22 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza amezunumzia mwonekano wa mwili wake na kusema kuwa hata yeye haelewi ni kwa nini kila siku anazidi kupungua.

Akiandika katika moja ya picha ambazo Mbosso alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diamond alionesha kushangaa kwake kutokana na kuendelea kupunguka kwa mwili wake na kila siku kuonekana kama kitoto.

Alisema kuwa si yeye tu anazidi kushangaa kutokana na mabadiliko hayo ya mwili wake bali pia hata Watanzania wote wamekuwa wakiibua maswali kama hayo.

“Halafu nimekuwa mdogo, kila siku nazidi kuwa mdogodogo. Hilo swala linawachanganya Watanzania wengi,” Diamond aliandika.

Jibu la Mbosso ndio liliwaacha wengi katika gumzo kubwa kwani walionekana kutolielewa.

Kwa kawaida wengi wanamjua Diamond kuwa wa miaka chini ya arobaini lakini kwa jibu la Mbosso alionekana kudokeza kuwa msanii huyo tajiri wa WCB Wasafi ana miaka zaidi ya 40 hivi.

“Kweli kaka kama hauna miaka 40 vile safi Sanaa,” Mbosso aijibu na kuwaacha wengi kweneye mataa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live