Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond ajibu mapigo ya Jux kwa Zari

Mondi Jux Jux na Diamond

Fri, 17 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diamond Platnumz; ni staa wa muziki nchini Tanzania ambaye kwa sasa ni stori kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akijiachia kimapenzi na mrembo aitwaye Karen anayesemekana ni ex wa msanii mwenzake, Juma Jux aliyedaiwa kutua kwa Huddah wa Kenya.

Ishu hiyo inajiri wiki kadhaa baada ya Jux naye kujiachia na baby mama wa Diamond ambaye ni Zari The Boss Lady; tukio ambalo lilichukua nafasi pale Beach-Kidimbwi jijini Dar wakati wa uzinduzi wa Video ya Simuachi ya Jux.

Tukio la Jux na Zari liliteka mitandaoni ambapo ilibidi jamaa huyo afafanue kuwa, Zari si mpenzi wake bali ni marafiki tu.

Kitendo cha Diamond kujiachia na mrembo huyo wa Jux inasemekana ni aina f’lani ya kulipiza kisasi baada ya tukio la Zari ili kuoneshana ubabe wa ujana; Kwamba, ukinichukulia ex-wangu na mimi nakuchukulia ex-wako!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live