Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond aitolea uvivu Ziiki Media

Diamond Mtv Diamond aitolea uvivu Ziiki Media

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mara nyingine tena Kampuni ya Usambazaji Muziki ya Ziiki Media, inaingia kwenye mgogoro na msanii wa Bongo Fleva, awamu hii Diamond ametoa tuhuma dhidi yao akidai kuwa Ziiki Media imezuia wimbo wa Lavalava 'Kibango' kutolewa siku ya leo.

"Ni masikitiko kuona kampuni ya Ziiki inauzuia wimbo wa Lavalava Kibango, kutoka siku ya leo na kulazimisha kutoa tarehe wanayotaka wao tena mwezi ujao pasipo sababu ya msingi". Ameandika Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram

Hata hivyo Diamond amedai kuwa tangu waikatalie kampuni hiyo kununua hisa za umiliki wa lebo ya Wasafi, Ziiki imekuwa ikiwavuruga kwenye utoaji wa nyimbo na kujaribu kuua kimuziki wasanii wa Wasafi.

Diamond ameendelea na kudai kuwa kampuni hiyo imewaonya Wasafi kuwa endapo wimbo huo wa Lavalava utatoka leo utashushwa na kuhakikisha watu hawaupati popote.

"Ziiki wameahidi kwamba endapo siku ya leo tutapandisha wimbo wa Lavalava Kibango wataushusha kila platfors na kuhakikisha watu hawaupati popote ". Ameandika Diamond

Aidha Diamond amesema imefanya waone kuwa Ziiki wanachuki na wasanii wa lebo ya WCB, hivyo imewalazimu kusughulikia jambo hilo kisheria.

Mbali na malalamiko hayo Diamond amewatoa hofu mashabiki wa muziki kwa kueleza kuwa wimbo huo wa Lavalava ambao yeye ameshirikishwa utatoka leo.

"Msijali mashabiki zetu Kibango Lavalava x Diamondplatnumz tunaitoa leo na wakiitoa kwa platforms tutawasambazia hata kwa WhatsApp ombi langu support kubwa ili wajue kuwa mashabiki wanataka ngoma sio propaganda waachie ngoma zitoke". Ameandika

Utakumbuka kuwa kuliwahi kuzuka tetesi zikidai Diamond ni mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo ya usambazaji muziki, hata hivyo na tetesi hizo zilikanushwa Septemba 2023, na Meneja wa kampuni hiyo, Camilla Owora kwa kutolea ufafanuzi wa kukanusha uvumi huo na kueleza kuwa Diamond siyo mmiliki, siyo mwekezahi wala hana hisa zozote Ziiki Media.

Mbali na Diamond, mwaka 2023, Harmonize pia amewahi kuwatuhumu Ziiki kutomlipa pesa zake jambo lililopelekea aombe msaada wa kupata haki serikalini, na Agosti 2022 mwanamuziki Vanessa Mdee kupitia ukurasa wake wa Instagram aliitolea uvivu Ziiki kwa kutaka alipwe pesa zake. .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live