Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond aibukia kwenye kampeni za Raila Odinga

JET  DIAMOND Diamond Platnumz

Sat, 6 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muungano wa Azimio la Umoja umemualika mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kutumbuiza katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni katika uwanja wamichezo wa Kasarani Jumamosi, tarehe August 6, 2022.

Raila Odinga ameongoza kampeni yake ya mwisho katika uwanja wa Kasarani huku Naibu Rais William Ruto akifanya kampeni zake katika eneo tofauti mjini Nairobi wakati kampeni zikifikia ukingoni Jumamosi hii.

Mikutano ya kampeni ya Jumamosi inakamilisha kampeni za kisiasa za wagombea wote wa uchaguzi kulingana na sheria na muda wa mwisho na sheria za Tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC)

Kabla ya kuelekea Nairobi Diamond ambaye alikuwa ameambatana na mwanaye Tiffah alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live