Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond aibukia kwa Alicia Keys

Alicia+keys+pic Diamond aibukia kwa Alicia Keys

Tue, 15 Sep 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By KELVIN KAGAMBO Licha ya kwamba tayari ameshafanya mambo mengi makubwa ya kuvunja rekodi, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz ameendeleza desturi yake hiyo baada ya jana jina lake kutajwa kwenye albamu ya mwanamuziki wa Marekani, Alicia Keys.

Kupitia kwenye moja ya akaunti za mtandao wa kijamii wa Twitter zilizojikita kwenye kutoa habari za msanii Alicia Keys, liliwekwa tangazo la albamu yake anayotarajia kuiachia Septemba 18 mwaka huu na wakatajwa miongoni mwa wasanii alioshirikiana nao na hapo ndipo jina la Diamond lilipochomoza.

“Albamu ijayo ya Alicia Keys ambayo inaitwa Alicia itakuwa na nyimbo 15 na atakuwa ameshirikiana na wasanii kama vile Miguel, Khalid, Sampha, Diamond Platnumz, Snoh Aalegra na Jil Scott!” imeandikwa katika ukurasa huo.

Lakini pia baada ya post hiyo, post nyingine iliwekwa ikionesha nyimbo zote 15 katika Albamu hiyo ambapo wimbo wa Alicia Keys na Diamond ni wimbo namba nne unaoitwa Wasted Energy.

Mbali na kuwemo kwenye albamu, pia jina la Diamond limejitokeza kwenye Playlist ya Alicia Keys ya mtandao wa kusikiliza muziki wa Spotify, ambapo aliweka nyimbo 15 anazosikiliza sana, na mbili kati ya hizo ni za Diamond.

Ngoma hizo ni African Beauty ya Diamond ft Omarion (msanii wa Marekani), na Nana ya Diamond ft Mr. Flavour (msanii wa Nigeria)

Chanzo: mwanaspoti.co.tz