Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond afunguka sababu ya kutumia 'Private Jet'

Diamond Ndege Trs(2).png Diamond afunguka sababu ya kutumia 'Private Jet'

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diamond Platnumz ni mmoja wa wasanii barani Afrika ambao usafiri na vifaa vya bei ghali zikiwemo ndege za kibnafsi na magari ya dhamani ya juu wakati anapozuru taifa lolote kufanya tamasha la muziki.

Ndege ya kibinafsi ilitajwa kuwa ya gharama mno wakati zinapotoa huduma za kusafiri ila kwa mwamuziki Diamond ndege hizi ndio bora zaidi kwa kuwa zinasafiri kwa kasi na kwa muda ufaao.

Baada ya mahojiano ya moja kwa moja na mwanablogu wa Wasafi Media ambayo pia ni mojawapo ya kampuni zinazomilikiwa na nyota huyu wa Bongo alifunguka na kusema anapendelea kutumia ndege ya kibnafsi kwa maana zinamsafirisha wakati anapopendelea.

"Napenda sana kupaa kwa kutumia ndege za kibnafsi kwa maana zinauwezo wa kusafiri wakati wowote ule ukilikanisha na ndege  za kawaida ambazo lazima ukate tikiti na pia zina wakati wao wa kusafiri", alisema.

Diamond alidokeza kwamba Ndege ya kibnafsi zinampa wakati mzuri wa kusafiri wa kupumzika  na kufanya sherehe pamoja na marafiki wake kwa kuwa muundo wa ndani ni tofauti na ndege za kawaida.

"Mimi ni msanii mkubwa ndio maana safari zangu zimekuwa mingi nisipotumia ndege ya kibnafsi nitakosa kuhudhuria nyinginezo,rubani wa ndege hizi pia yuko tayari kunisafirisha kwa wakati wowote iwe usiku au mchana," alisema.

Msanii huyu alielezea haya wakati alipotua kwenye uwanja wa ndege Kahama,kuudhuria tamasha la Wasafi Festival baada ya kumaliza ziara yake mjini Nairobi kwa tamasha la Oktobafest.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live