Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond aendelea kutimiza ahadi zake kwa mashabiki

Diamondplatnumz 1690377883709.jpeg Diamond aendelea kutimiza ahadi zake kwa mashabiki

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa nyimbo za Bongofleva nchini Tanzania Diamond Platnumz maarufu Simba ameendelea kufanikisha wajibu wake na kutimiza ahadi alizoahidi mashabiki katika sanaa yake ya muziki.

Mwezi Juni, mwimbaji huyo alivunja kimya chake kwa kukaa kwa muda mrefu bila kutoa wimbo wowote ambapo aliahidi mashabiki kuwa watarajie mengi kutoka kwake mwezi uliokuwa unafuata, yaani mwezi Julai kwani alikuwa akiangazia maswala na vyombo vya habari wakati huo.

Diamond, alisema kuwa kuwanzia Julai, kutanyesha mvua ya mawe katika muziki na ambapo kufika sasa tayari ametoa nyimbo mbili na ambazo kulingana na utafiti wa Charts, nyimbo hizo zimekuwa kileleni mwa nyimbo zilizotazamwa sana YouTube.

Katika kipindi hicho cha mwezi mmoja, Simba alitoa wimbo unaojulikana kama Enjoy, kwa kumshirikisha Jux, ambapo kwa kusaidia na mpenzi wake Zuchu, wimbo huo ulisambazwa katika mitandao yote ya kijamii na hivyo kupata umaarufu zaidi.

Wimbo huo wa Enjoy, uliibua hisia mseto katika mitandao ya kijamii, ambapo baadhi ya wanamitandao walidai kuwa wimbo huo Diamond alinakili mdundo wake kutoka kwa msanii mwingine.

Ni katika mwezi huo pia, ambapo wimbo unaofahamika kama Baby, pia uliweza kutikisa anga na kuwa na watazamaji wengi katika mtandao wa TikTok, ambapo mwimbaji huyo aliweka bayana kuwa atazidi kutoa nyimbo zaidi siku za hivi karibuni.

Simba amemkosoa vikali msanii mwenzake wa nyimbo za bongo Ali Kiba, ambaye alimfokea katika mtandao wake wa Twitter kuwa amwache kwa maana kila wimbo anotoa anatoa kwa mpango na wala hapurukuti ovyo.

Mwimbaji huyo waaidha ameelekeza hatma ya moyo wake kwa mpenzi wake Zuchu, ambapo alikiri kuwa anaweza kusitisha muziki ili kulithibiti na kulihimarisha penzi lao kwani amejihisi kufanya mengi katika muziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live