Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond aanika sifa za chopa yake "Ni tofauti na helkopta nyingine Afrika"

Mondi Helicopter .jpeg Diamond aanika sifa za chopa yake "Ni tofauti na helkopta nyingine Afrika"

Sat, 13 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kwenye mahojiano yake juzi Alhamisi, Agosti 11, 2022 katika kipindi cha #TheTouchDown cha Metro FM, nchini Afrika Kusini kwa mara ya kwanza ameweka wazi juu ya Helikopta yake aliyonunua na kubainisha kuwa chombo chake hicho kina uwezo wa kuruka usiku tofauti na helikopta nyingi ambazo zina uwezo wa kuruka mchana pekee.

Diamond amesema, Helikopta hiyo aliyonunua ndio ya kwanza kati ya Helikopta chache Afrika Mashariki zenye uwezo wa kuruka usiku kwani Helikopta nyingi zinaruka mwisho saa 12 jioni.

"Nilinunua kwanza ndege, jana nimetoka kununua Helikopta, na baada ya wiki nne itakuwa tayari imekuja Tanzania. Na Helikopta yangu ni kati ya Helikopta chache Afrika Mashariki zenye uwezo wa kuruka usiku yaani baada ya jioni SAA 12." - ameeleza Diamond.

Wataalam wa masuala ya ndege wanasema Helikopta nyingi huwa haziruki usiku kutokana na kuwa zinaruka umbali wa chini tofauti na ndege hivyo kuhatarisha maisha ya waliopanda. Helikopta haishauriwi iruke usiku kwa sababu inaweza ikagonga mwamba, mti mkubwa n.k tofauti na ndege ambayo inakuwa anga ya juu.

Helikopta zinazotajwa kuwa zina uwezo wa kuruka usiku ni zile za Kijeshi, ama za huduma (msaada kiafya, moto n.k) ambapo zinakuwa na vifaa mahususi kwa ajili ya kuona usiku. Hivyo @diamondplatnumz Helikopta yake amesema ni moja kati ya ambazo zina huo uwezo wa kuruka usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live