Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Zuchu sasa wanalishana kwa ulimi

DIAMOND ZUCHU TENA.png Diamond, Zuchu sasa wanalishana kwa ulimi

Sat, 27 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya wenyewe kutoweka wazi kuwa na mahusiano lakini vithibitiasho vinavyodhirisha kama ni mtu na mtuwe vinazidi kuvuja deile.

Iko hivi, kuna kipande kipya cha video kinachomuonesha Diamond na Zuchu wakiwa kwenye katika Uwanja wa Ndege wa Songwe na katikati yao yupo chawa Pro Max, Baba Levo.

Kinachoendelea hapo ni Diaomond kuweka kitu mdomoni kama keki hivi kisha kupeleka mdomo wake kwa Zuchu na bila hiyana mtoto wa kizanzibari akapoke kwa ulimi ikaisha hivyo.

Bahati mbaya au nzuri kwao, sauti iliyokuwa inasikika kwenye video hiyo haihusiani na tukio lililokuwa linaendelea hivyo unaweza tu kuona watu wanagusanisha ulimi huku Baba Levo akionekana kufurahia kitendo hicho alichokishuhudia akiwa 'ziro distance' na mastaa hao wakubwa Bongo.

Hii sio mara ya kwanza kwa wawili hawa kuoneshana vitendo vya kimahaba, kama unakumbuka juzikati wakiwa kwenye shoo ya uzinduzi wa albamu ya Love Sounds Different ya Barnaba katika Ukumbi wa Mlimani City, waligandana jukwaani kimahaba na mambo yalikuwa fire.

Tuwasubiri wenyewe siku isiyo na jina huwenda wakaweka wazi kila kitu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live