Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond: Wasanii wa Nigeria ni wanafki, tusiwaige

Diamond Zuchu K Diamond: Wasanii wa Nigeria ni wanafki, tusiwaige

Wed, 17 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewataka wasanii wa Bongo kuacha tabia ya kuwekeana mabifu ya ukweli na badala yake washirikiane kibiashara.

Diamond amezungumza hilo alipokuwa kwenye usiku wa uzinduzi wa albamu ya Elius Barnaba inayokwenda kwa jina la Love Sound Different katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar usiku wa kuamkia Agosti 17, 2022.

“Wenzetu wa Nigeria wanapendana sana lakini nje wanaonesha mabifu, ni wanafki. Wanafanya shoo pamoja na wanapendana. Tunatakiwa na sisi kuwekeana mabifu ya kibiashara lakini kwa uhalisia tunakuwa tunapendana,” alisema Diamond.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live