Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Wasafi waula

6e10e7b60db9e7b78598ed58cd5cd415.jpeg Diamond, Wasafi waula

Wed, 19 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KAMPUNI ya muziki ya Warner imetangaza ushirikiano mpya na msanii namba moja Afrika Mashariki Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ na lebo yake ya Wasafi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Warner kupitia mtandao wao jana, ushirikiano huo utamsaidia Diamond na wenzake kupata hadhira kubwa duniani kote ambapo pia, lebo ya Wasafi itashirikiana masuala mbalimbali ya muziki na Warner Afrika Kusini na Ziiki Media.

Ushirikiano huo mpya wa kimkakati wa 360 umelenga kuhakikisha Warner Music, Diamond Platnumz, Ziiki Media na wasanii wa WCBWasafi wakishirikiana kwenye utoaji wa nyimbo mpya, mambo mapya yanayoendelea duniani, ushirikiano wa chapa, mikataba ya moja kwa moja na usawazishaji.

“Nimeijenga Wasafi kwa muda mrefu na ninaamini kwamba Warner na Ziiki ni wadau sahihi wa kutusaidia kukua na kufikia malengo. Na pia ninaangalia uwezekano wa kuingia kwenye mtandao wa Warner mwenyewe.

Tuna mipango mingi mikubwa, siwezi amini namna nitakavyoshiriki muziki wangu na mashabiki duniani,”alisema Diamond.

Rais wa Warner Alfonso Perez-Soto alisema kipaji cha muziki cha Diamond Platnumz hakipingiki na amekuwa mmoja wa wasanii waliofanikiwa zaidi Afrika. Juu ya hayo, am-

ethibitishwa kuwa mfanyabiashara mzuri, kwani amekua WCB-Wasafi kuwa lebo ya rekodi ya kutisha.

“Muziki wa Afrika Mashariki na Kati umekua kwa miaka michache iliyopita na tunaamini kwa kufanya kazi pamoja, tunaweza kusaidia kumtangaza Diamond na wasanii wake kwa mashabiki zaidi ulimwenguni, na kutambulisha muziki wa Bongo Fleva kwa hadhira pana,”alisema.

“Ushirikiano huu wa 360 unaanzisha njia mpya ya kushirikiana na wasanii Afrika na azma yetu ya kuleta vipaji vya Kiafrika kwa

ulimwengu wote. Ningependa kuwashukuru WM Afrika Kusini na Ziiki Media kwa msaada wao mzuri katika kufanikisha mpango huu. “ Nyota huyo ni miongoni mwa wasanii wa Afrika Mashariki wanaofanya vizuri kwa muda mrefu na kupitia lebo yake ya Wasafi wanaofurahia mafanikio ni Abdul Iddi ‘Lavalava’, Mbwana Kilungi ‘Mbosso’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Zuhura Othman ‘Zuchu’ na Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’.

Chanzo: www.habarileo.co.tz