Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond: Tulitofautiana kidogo na Rayvanny lakini...

Diamond&Rayvanny Diamond: Tulitofautiana kidogo na Rayvanny lakini...

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amesema, wakati aliyekuwa msanii wake Rayvanny anataka kuondoka WCB walitofautiana kidogo lakini hata hivyo, walishamaliza.

Diamond alizungumza hayo kwenye jukwaa la Acces lililowakutanisha wadau wa sanaa jijini Dar ambapo, Mfalme huyo wa Bongo Fleva, alikuwa miongoni mwa wazungumzaji na alipokuwa akizungumza kuhusu fursa za mitandao ndipo alipomgusia Rayvanny.

"Rayvanny kama mnavyojua alindoka WCB namshukuru Mungu ananiheshimu, tulitofautiana kidogo kama unavyojua mnapoachana kunakuwa na vitu wakati mwingine inaweza visiende sawa lakini namshukuru Mungu tulimaliza vizuri.

"Kama unaona ameenda WCB anafanya kazi Next Level anafanya kazi na Mziki na wimbo wake wa kwanza amenishirikisha mimi," alisema Diamond.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live