Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, TRA sasa mambo fresh

Diamond Platnumz 34 1140x640.jpeg Diamond Platnumz

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika mahojiano aliyoyafanya msanii Diamond Platnumz kupitia Wasafi Media, aliwahuhumu Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania (TRA) kuwa inamuandama, lakini leo ameelea kuwa wameyamaliza.

Leo Alhamisi Desemba 5, 2022, kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Diamond anmeandika;

"Siku ya jana (Jumatano) nilipata wasaa mzuri wa kuhudhuria Makao Makuu ya TRA, kuzungumza nao na kupata elimu mbalimbali juu ya kodi.

"Kikao kilienda vyema na nikapewa elimu mbalimbali ambazo zitaongeza ustawi bora wa kampuni na biashara zetu, lakini pia namna sahihi ya kuendelea kuchangia pato la Taifa.

"Kipekee nimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwa kutupa Serikali sikivu, lakini pia nimshukuru Waziri wa Fedha na Mipango Mh @mwigulunchemba, Kamishna mkuu TRA Alphayo J. Kidata kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kwenye kuhakikisha kwamba TRA inaendelea kuwa mlezi bora kwenye ustawi wa biashara na wafanyabiashara."

Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Wasafi Nasibu Abdul Juma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live