Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond: Siwezi, sikubali kuwa balozi wa bidhaa bandia

77245 Pic+dai

Wed, 25 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Dili za ubalozi zimeendelea kumtembelea mwanamuziki maarufu nchini Tanzania, Diamond Platnumz na leo Jumatano Septemba 25, 2019 amesaini mkataba wa kuwa balozi wa kampuni ya Bomet.

Katika mkataba huo Diamond amekuwa balozi wa sabuni ya unga ya Niceone inayozalishwa na kusambazwa na kampuni hiyo.

Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Anne Semtumbi amesema wameamua kumpa nafasi hiyo Diamond kutokana na uchapakazi wake na namna anavyojituma.

“Mikakati yetu kama kampuni ni kusambaa nchi nzima na kuwafikia Watanzania wengi, tumeona Diamond anaendana nasi kutokana na namna anavyojituma, ni mbunifu, mahiri na mchapa kazi,” amesema

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa balozi Diamond amesema amekubali kuingia makubaliano hayo baada ya kuthibitisha kuwa bidhaa hiyo ina ubora.

“Mungu amenijalia kufanya kwanza utambuzi wa bidhaa ninayoingia ubalozi kabla ya kukubali, ukiacha fedha nitakazopata nataka jamii yangu itumie kitu kilicho bora wasipate madhara halafu nipate lawama,” amesema

Pia Soma

Advertisement
Diamond atautumikia ubalozi wa sabuni hiyo kwa miaka miwili. Hata hivyo, kiasi cha fedha ambacho msanii huyo akakipata hakijawekwa wazi.

Chanzo: mwananchi.co.tz